Bendera ya kijani ya Kiarabu ya Libya,Jamahiriya. Rangi ya kijani, ambayo iliwakilisha Uislamu na Nadharia ya tatu ya Kimataifa ya Gaddafi, ikiorodheshwa katika Kitabu cha Kijani.
Muammar Gaddafi alipata kuwa kiongozi mkuu wa Libya tarehe 1 Septemba1969 baada ya kuongoza kundi la maofisa vijana wa jeshi la Libya dhidi ya mfalmeIdris I katika mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu. Baada ya mfalme huyo kukimbia nchi, baraza la mapinduzi (RCC) lililoongozwa na Gaddafi lilifuta utawala wa kifalme na katiba ya zamani na kuanzisha Jamhuri ya Kiarabu ya Libya, yenye kauli mbiu “uhuru, ujamaa na umoja”.[1][2]